Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Joe Biden ambaye alikuwa akizungumza na wananchi wa Marekani kuhusu tatizo la ubaguzi wa rangi nchini humo, ameongeza kuwa, miongoni mwa mambo muhimu katika uwanja huuo ni kuchunguza sababu zinazopelekea kuwepo mienendo tofauti dhidi ya wasio wazungu yakiwemo maamuzi yanayotolewa mahakamani.
Kuhusu suala la sera za kuzusha mifarakano katika jamii ya Marekani, Biden amesema atamshughulikia mtu yeyote anayeeneza sera za kuzusha hitilafu na mifarakano.
Rais huyo wa Marekani amedai kuwa, miongoni mwa masuala yaliyomfanya ashiriki katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais wa mwaka jana ni kuhuisha utukufu wa mwanadamu, fahari na uamunifu nchini Marekani.
Wapembuzi wengi wa mambo wanasema kuwa, ubaguzi wa rangi na fikra za kuwaona wazungu kuwa ndiyo kizazi bora zaidi zilipamba moto zaidi nchini Marekiani baada ya Donald Trump kushika madaraka ya nchi mwaka 2016 na kufikia kileleni baada ya mauaji yaliyofanywa na polisi wazungu wa nchi hiyo dhidi ya Mmarekani mweusi, George Floyd katika mji wa Minneapolis hapo tarehe 25 Mei 2020.
342/